Nenda kwa yaliyomo

Maziwa makubwa ya Amerika Kaskazini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pitio kulingana na tarehe 09:26, 5 Septemba 2009 na SieBot (majadiliano | michango) (roboti Badiliko: sco:Muckle Lochs)
Maziwa makubwa kati ya Marekani na Kanada

Maziwa makubwa ya Amerika Kaskazini ni jumla ya maziwa matano yanayotawanyika mfululizo kwenye mpaka kati ya Marekani na Kanada. Ziwa moja la Michigan pekee limo ndani ya Marekani.

Maziwa haya ni gimba kubwa la maji matamu duniani. Eneo lao linatosha kwa kuonekana kwa maji kujaa na kupwa.

Maziwa haya ni:

Maziwa makubwa jinsi yanavyoonekana kutoka angani


Maji hupita kuanzia Ziwa Superior na Ziwa Michigan kwenda Ziwa Huron; halafu kupitia mto Detroit kwenda Ziwa Erie; haafu kupitia maporomoko ya Niagara kwenda Ziwa Ontario; kutoka hapa maji hutoka katika Mto Saint Lawrence unaokwisha kwenye Bahari ya Atlantiki.

Kuna visiwa zaidi ya 35,000 ndani ya maziwa haya. Kisiwa cha Manitoulin katika ziwa Huron upande wa Kanada ni kisiwa cha ziwani kikubwa duniani chenye eneo la 2,766 km² na eneo hili ni kubwa kuliko maeneo ya Unguja (1,658 km²) na Pemba (980 km²) pamoja.

Makala hii kuhusu maeneo ya Marekani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Maziwa makubwa ya Amerika Kaskazini kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Wikimedia Commons ina media kuhusu: